riwaya za Fadhy Mtanga

HUBA

NI simulizi ya aina yake.  Imejaa visa vinayosisimua.  Inaakisi mapenzi ya kweli.  Mapenzi yasiyochuja hata katika nyakati ngumu.

Kwenye HUBA, kuna wahusika watakaozivuta hisia zako.  Watakaokushirikisha furaha na huzuni zao, katika kizungumkuti cha HUBA.

Kuna ZEDI kijana maridadi.  Anayevunja sheria za barabarani kwa kwenda mwendo mkali.  Anaposimamishwa na askari wa kike,  ZEDI anashindwa kuzizuia hisia zake.  Anazama katika HUBA.

Kuna JULY, msichana mrembo mno, mwenye staha za kutosha.  JULY mwenye mapenzi ya kweli kwa ZEDI.  Lakini ZEDI, hana muda naye kwa kuwa akili yake ipo kwa ROSE.

Kuna ROSE anayezama ghafla katika HUBA la ZEDI.  Je, atafanikiwa kuyapiku mapenzi ya kweli ya JULY?

Kuna JERRY na SHANIA, marafiki wa kweli daima.

Hii ndiyo HUBA, ukiufungua ukurasa wa kwanza, hakika hutokiweka chini, hadi ukurasa wa mwisho.

Kitabu cha HUBA kimetolewa mwezi Mei 2014.  Kinapatikana kwa kukiagiza moja kwa moja kwa namba 0715 599 646 ama 0754 599 646 ama kupitia barua pepe: fadhymtanga@gmail.com

KIZUNGUMKUTI

HAFSA Hashimu alikuwa na kila kitu chenye kumfanya ayafurahie maisha. Elimu nzuri. Kazi nzuri. Mume aliyempenda kwa dhati ya moyo wake. Alikuwa mwenye furaha ya ndoa yake.
Aliamini hakuna kitu kitakachoharibu furaha ya ndoa yao zaidi ya maradhi na kifo.
Aliamini hivyo, hadi jinamizi la Benito, rafiki yake wa kiume wakiwa shule ya sekondari lilipojitokeza na kumweka katika wakati mgumu zaidi.

Riwaya hii ilitolewa katika kitabu mwaka 2012

Chapa ya Pili inatarajiwa mwezi Julai 2014

Pia, kwa kuendelea kufaidi simulizi za Fadhy Mtanga, jiunge na ukurasa wake wa Facebook kwa anwani ya http://facebook.com/fadhymtangapage