Tuesday, March 28, 2017

Vile Ulivyo

Vile we' utembeavyo,
Kwa mikogo,
Ndivyo univutiavyo,
Si kidogo.

Vile unitazamavyo,
Ooh walah!
Ndivyo unimalizavyo,
Mie hoi.

Na rangi yako ilivyo,
Asilia,
Kwa namna ing'aavyo,
Yavutia.

Vile neno usemavyo,
Shamshamu,
Sauti ikutokavyo,
Kwa utamu.

Umbo zuri vivyo hivyo,
Mashaallah!
Linoge vile wendavyo,
Inshaallah.

Hata hivi nandikavyo,
Kwa utenzi,
Ndo hivyo nikuwazavyo,
Sijiwezi.

Fadhy Mtanga,
Mbeya, Tanzania.
Jumanne, Machi 28, 2017.

1 comment:

  1. Wao bonge la shairi.. nimependa mmmhhh utamu wa shairi umpata mshairi kama mtani wangu hapa

    ReplyDelete