Sunday, May 8, 2016

Ninyunyizie

Ninyunyizie,
Nami ninukie,
Harufu iwafikie,
Wivu uwazidie,
Donge liwapalie.

Wenye husda walie.

Wenye ngebe waumie.

Ngendembwe ziwaishie.

Ninyunyizie,
Nizidishie.

Marashi ya upendo.

Fadhy Mtanga,
Mafinga, Iringa.
Jumapili, Mei 8, 2016.

2 comments:

  1. Mnyunyuzo nahisi umekufikia
    yanukiayo kama marashi ya Pemba
    Ahsante kwa shairi mtani!

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana da Yasinta, msomaji wangu usiyenichoka pamwe uvivu wangu huu.

    ReplyDelete