Thursday, December 31, 2015

Mwaka UnapokwendaKumbe mwaka unakwisha,
Kalenda yaniambia,
Mwaka unapokwenda,
Basi uende peke yake,
Usiende na mapenzi yangu,
Usiende na furaha yangu.

Miezi kumi na mbili,
Ina mengi sana,
Siku mia tatu sitini na tano,
Basi ziende peke yake,
Zisiende na mapenzi yangu,
Zisiende na furaha yangu.

Wiki zimekatika katika,
Zikaenda zake,
Wiki hamsini na mbili,
Basi ziende peke yake,
Zisiende na mapenzi yangu,
Zisiende na furaha yangu.

Maisha lazima yaendelee,
Chambilecho wahenga,
Zichanike jamvi zivunjike koleo,
Basi viende peke yake,
Visiende na mapenzi yangu,
Visiende na furaha yangu.

Nenda mwaka nenda zako,
Ewe mwaka nenda zako,
Lakini unapokwenda,
Basi uende peke yake,
Usiende na mapenzi yangu,
Usiende na furaha yangu.

Fadhy Mtanga,
Mbeya, Tanzania.
Alhamisi, Disemba 31, 2015.

2 comments:

  1. Nakuambia yaani mwakaumekwisha
    Na mengi hayajatimizwa
    La muhimu ni kumshukuru Mungu kwa yote na pia tuendelea kumuuomba masaa yaliyobaki ili tuuone mwaka 2016.

    ReplyDelete
  2. bro uko vizur san vin tupe vya 2016 bc

    ReplyDelete