Thursday, December 3, 2015

Mpenzi kalamu

Salamu,

Ee wangu muhashamu,
Ulo kwangu muhimu,
Tena daima dawamu,
Aaah wanipa raha!

Niliitupa zamu,
Kisa eti majukumu,
Ni nini huu wazimu,
Aaah mbona karaha!

N'sharejea mumu humu,
N'shaitema ile sumu,
Wewe u wangu mwalimu,
Aaaah mbona furaha!

Mpenzi wangu muhimu,
Mpenzi wangu kalamu,
Niondolee magumu,
Aaaah nipate siha!

Pokea zangu salamu!

Fadhy Mtanga,
Tukuyu, Mbeya.
Alhamisi, Disemba 3, 2015.

4 comments:

 1. Ni furaha ilioje kwa kusoma huu ujumbe,
  Akili na mwili vyote vimefurahia
  Karibu, katibu tena....karibu sana katika ulimwengu huu

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ahsante sana da Yasinta kwa kuwa msomaji wangu usiyenichoka pasi kujali uvivu wangu wa kuandika.

   Delete
 2. Kukuchoka haipo katika akili yangu
  Mashairi ni moja ya maisha yangu
  Kwa hiyo hii ilikuwa ni furaha kubwa kwangu
  Na natumai sasa utadumu.

  ReplyDelete
 3. Andika sana ..tunakufuata taratibu ndugu yetu

  ReplyDelete