Friday, August 15, 2014

Nayapenda maisha

Nayapenda maisha,
Kwa furaha yanipayo,
Kwa huzuni yanileteayo.

Nayapenda maisha,
Kwa mapenzi niyapatayo,
Kwa chuki zinipitiazo.

Nayapenda maisha,
Kwa mafanikio nipatayo,
Kwa changamoto nizipatazo.

Nayapenda maisha,
Kwa jitihada nilizonazo,
Kwa uvivu niupatao.

Nayapenda maisha,
Kwa ndugu wema nilionao,
Kwa ndugu wanichukiao.

Nayapenda maisha,
Kwa marafiki wema niwapatao,
Kwa wanafiki watokeao,

Nayapenda maisha,
Kwa afya njema niliyonayo,
Kwa maradhi yanipitiayo.

Nayapenda maisha,
Kwa akili nilizonazo,
Kwa umbumbumbu nilionao.

Nayapenda maisha,
Kwa imani na dini niliyonayo,
Kwa kutikiswa nikupitiako.

Nayapenda maisha,
Kwa maono na dhamira niliyonayo,
Kwa kukata tamaa nisikokuwa nako.

Nayapenda maisha.

Nayapenda sana.

Fadhy Mtanga,
Kabwe, Mbeya.
Ijumaa, Agosti 15, 2014.

8 comments:

 1. Nayapenda maisha kwani ni mara moja tu mtu huishi...nayapenda maisha...nimependa hizi tungo

  ReplyDelete
 2. Nayapenda maisha...i luv it keep it up.

  ReplyDelete
 3. Nayapenda maishaa
  Yenye mengi yasoisha
  Yasombio yakakwisha
  Nayapenda maishaa

  Nayapenda maishaa
  Tamu chungu zisokwisha
  Ndo furaha ya maisha
  Nayapenda maishaa

  Matamu ukipatia
  Chungu sana ukikosea
  Alokifani hakuna
  Nayapenda yomaisha

  Hakuna alokifani,maisha kuyapatia,
  Wote humu ni wageni,ninjia tu twapitia
  Ni matamu kupitia,nayapenda yomaisha

  ReplyDelete
  Replies
  1. Nayapenda maisha,
   Mengiye hayatoisha,
   Japo hayatotosha.

   Delete