Sunday, September 8, 2013

Kama nyota za angani

Kama nyota za angani,
Usiku zinavyong’aa, ndivyo penzi langu kwako,
Mapenzi yamenijaa, huba tele juu yako,
Wala sikati tamaa, mimi ndiye mali yako.

Kama nyota za angani,
Usiku zinavyong’aa, ndivyo ninavyokupenda,
Kwako mefika haswaa, kwingine siwezi kwenda,
Maneno nayakataa, yaso ubani yavunda.

Kama nyota za angani,
Usiku zinavyong’aa, wewe ndo mpenzi wangu,
Bora wakinishangaa, sitoweza peke yangu,
Kamwe sijihisi njaa, uwapo pembeni yangu.

Kama nyota za angani,
Usiku zinavyong’aa, daima nitakuenzi,
Siwezi kukuhadaa, ewe wangu laazizi,

Moyoni ushanikaa, we ndiwe wangu mpenzi.

Fadhy Mtanga,
Kijitonyama, Dar es Salaam.
Jumapili, Septemba 8, 2013.

2 comments:

  1. Mtani wa mimi! Nakubaliana nawe..kupenda kuna raha zake na kweöi kupenda hakuchagui.

    ReplyDelete
  2. Mtani ni kweli kabisa. Pia nakushukuru sana ni miaka 6 toka uanze kuwa msomaji wangu. Najivunia kwa kutonichoka kwako.
    Pamoja sana mtani.

    ReplyDelete