Monday, August 26, 2013

Yeye yule

Nipo kilimani ninaranda,
Wala singoji Peugeot kupanda,
Ninamngoja ninayempenda,
Moyo wangu alouchukuwa.

Aloniponya changu kidonda,
Alonifanya n'ache kukonda,
Moyo wangu mwenye kuulinda,
Kwayo mahaba ninayopewa.

Mpenzi wangu nayempenda,
Kwa silabi irabu na inda,
Ambaye bilaye swezi enda,
Juu yake ndo nishanogewa.

Kwa dhati ya moyo nampenda,
Wala hakuna wa kumshinda,
Namuwaza kila nakokwenda,
Penzi moyoni limeridhiwa.

Fadhy Mtanga,
Arusha Tanzania,
Jumatatu, Agosti 26, 2013.

1 comment:

  1. Hapo ..."kwa dhsti ya moyo nampenda
    Wala hakuna wa kumshinda,
    Namuwaza kila nakokwenda,
    Penzi moyoni limeridhiwa." Hapa patamu kweli mtani wa mimi:-D

    ReplyDelete