Tuesday, May 28, 2013

Taratibu basi!

kitaka kunipenda nipende taratibu,
Ukizidisha utaniuwa mwenzio!
Ukitaka kunipa raha basi iwe taratibu,
Ukizidisha utaniuwa mwenzio!

Ukitaka kuniumiza niumize tu kidogo,
Ukizidisha utaniuwa mwenzio!
Ukitaka kunitesa sikuzuwii ila taratibu,
Ukizidisha utaniuwa mwenzio!

Moyo wangu, moyo wangu uendee taratibu,
Ukizidisha waniletea masahibu!
Usiku silali ukiniuliza we ndo sababu,
Taratibu basi utaniuwa mwenzio!

Moyo wangu, moyo wangu unauadhibu,
Basi fanya japo taratibu!
Niondolee madhila yaliyozidia hesabu,
Utaniuwa mwana wa mwenzio!

Taratibu, twende taratibu basi taratibu,
Nitese tu kidogo ukipata sababu!
Ukizidisha moyo wangu wauharibu,
Ukizidisha utaniuwa mwenzio!

2 comments:

 1. Shairi la leo ni bonge la ujumbe,
  Nashisi ujumbe umemfika muhusika,
  Ila kwa kweli umenigusa mno mno,
  Ahsante kwa shairi hili lenye ujumbe maridhawa
  Na ahsante kwa kuandika shairi kwani muda sasa umepita.

  ReplyDelete
 2. Ahsante sana mtani wangu kwa kuwa msomaji usiyechoka wa tungo zangu.

  ReplyDelete