Wednesday, March 13, 2013

Hodi hodi!

Hodi,
Hodi hodi jamani nimerejea,
Mwana mpotevu niliyepotea,
Kwenye upweke nilielea,
Sasa ninarejea.

Hodi,
Hodi jamani nipokeeni,
Niruhusuni niingie ndani,
Msinipige faini japo hamsini,
Sasa nimerejea.

6 comments:

 1. Karibu,
  karibu karibu miwili mikono twakupokea,
  Tena kwa furaha isiyo kifani umepokelewa,
  Mengi twajua tutayapatakutoka kwako
  Na wala hutapigwa faini
  Karibu sana karibu sana:-)

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ahsante sana da Yasinta kwa kunikaribisha kwa mikono miwili

   Delete
 2. Vipi waipiga hodi, kitoka huna kuaga,
  Una za peke kusudi, faniyo chinii ibwaga,
  Si bora wende sirudi, kuliko kuzugazuga,
  Hapa wiki haizidi, huyo ushachanja mbuga!


  ReplyDelete
  Replies
  1. Wala sifanyi kusudi, Hallyie leo nakwambia,
   Ujuwe ninayo midadi, shairi kuwaandikia,
   Lakini huwa inanibidi, kazi za watu kukazania,
   Sitaki kuvunja ahadi, shairi nitawaandikia.

   Delete
 3. diwani fadhili pole na yako shughuli
  kiswahihili kukakuzi,kupitia ushairi
  nasi tulo nyuma yako twataka dumisha hilo
  hongera kwa yako hazi
  UKUTA kagera twakupongea kwa juhudi uzifanyazo
  kaka ongeza juhudi
  Lugha yetu adhimu kuienzi
  barikiwa sana

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ukuta Kagera, ninayo shukrani ya dhati kwa kupita kwenu katika blog yangu. Kwa pamoja tunayo dhima ya kukienzi na kukisambaza Kiswahili. Kwazo njia bora zaidi, ushairi u mojawapo. Karibuni sana.

   Delete