Monday, September 24, 2012

Wewe pekee

Nitakupa bega langu uliegamie,
Nitakupa mdomo wangu usemee,
Nitakupa masikio yangu usikilizie,
Nitakupa miguu yangu utembelee,
Kwa kuwa nakupenda sana.

 Dunia nzima nitaiambia isikie,
Tuzo ya thamani ndiwe uistahilie,
Hatokei mtu yeyote wewe akufikie,
Maishani wacha tu nikufurahie,
Uzuriwo umeshinda kawaida.

 Upo kwangu ya nyuma usiyawazie,
Mungu kanionesha wewe nikuchague,
Yanifanya daima wewe nikufikirie,
Penzi lenye thamani nikugaie,
Maana kwangu umeshatosha.

 Wewe pekee!

 Fadhy Mtanga,
Mbeya, Tanzania.
Jumatatu, Septemba 24, 2012.

4 comments:

  1. wow! bonge la ujumbe. Ningeandikiwa mimi ngefurahi kwali ningeuprinti na kuweka. Yaani nimeishiwa hata cha kusema ntaharibu naogopa..

    ReplyDelete
  2. Nyamweya Bw' OmariOctober 26, 2012 at 3:11 PM

    Sawasawa... Ninakiri ubingwa uliojionyesha hapa... Heko zangu n'akupa...

    ReplyDelete