Wednesday, September 28, 2011

Siku nyingi sana

Hakika sijaandika, nanyi hamjanisikia,
Ghafula nikakatika, bila hata kuwambia,
Wengi mkahamanika, nini kimenitukia,
Maswali yakawashika, vipi nimewakimbia,
Siku nyingi sana!

Wapi nilikofichika, hakuna wa kuwa'ambia,
Wapo walokasirika, bakora kunishikia,
Shimoni leo natoka, sitaki kosa rudia,
Mpate kuburudika, yote lowakusanyia,
Siku nyingi sana!

Nyote hapa kusanyika, nianze wahadithia,
Kunako zangu pilika, yote nilojionea,
Hakika tafurahika, khasira kuwaishia,
Hatungoji pambazuka, hivi ndo twajianzia,
Paukwa......!!!

5 comments:

 1. Bado,...

  ....``Siku nyingi sana!´´.:-(

  Wadau WAKIJIWE tupo lakini!
  Hata ukitufukuza labda tutakuja na jina la bandia!:-)

  ReplyDelete
 2. Habari za siku.
  Kama mwanablogu kutoka Tanzania,nakuomba kushiriki kuchangia Mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).

  Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya
  http://blogutanzania.blogspot.com/
  kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.
  Ahsante
  Luiham Ringo.

  ReplyDelete
 3. @ fadhy...

  Silete zako 'paukwa', khadithi kutuzugia
  Unahitaji kunyukwa, mikwaju ikakwingia
  Kwa 'pilato' hapelekwa, jalada kufungulia
  Siku nyingi sana!

  ReplyDelete
 4. Hakika ni siku nyingi sana,lakini twafurahi kuwa umegundua kuwa ni siku nyingi na umekuja kutusalimia...Ila siku nyingine tutakupeleka mahakamani:-)

  ReplyDelete