Tuesday, April 19, 2011

Mawazoni mwangu

Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.

Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.

4 comments:

 1. Fuata mtima wako,
  Na amini kwa dhati,
  Wala hujakosa ukamilifu,
  Fuata mtima wako.

  Ni ishara nzuri kumweka mawazoni pia ndotoni,
  Kwani ipo siku mtaja kuwa pamoja.
  Kila la kheri mtani.

  ReplyDelete
 2. Tafuta mpenzi wa kulipia akutulize roho kidogo Mkuu! Si nasikia wakulipia hawasumbui moyo namna hii?:-(

  ReplyDelete
 3. Usahauri wa mtakatifu......!!!

  ReplyDelete