Saturday, March 12, 2011

Unanikumbuka?

Unanikumbuka?
Hivi nivyoadimika,
Kitambo sijasikika,
Tungo sijaziandika,
Wewe nikakutumia.

Kwani waniwaza?
Ukimya kukuumiza,
Yeyote kumuuliza,
Apate kukueleza,
Nini kimenitokea.

Kwani watamani?
Nitoke huku shimoni,
Nikiseme mdomoni,
Furaha iwe moyoni,
Moyowo ukatulia.

Nini unachokipenda?
Roho iache kudunda,
Homa sikupe kukonda,
Ujuwe ninakupenda,
Upendo ulozidia.

Wanitaka nikwambie?
Moyo wao utulie,
Wengine wanisikie,
Nawe uufurahie,
Upendo ulozidia.

Niambie basi!

4 comments:

 1. Ahsante kwa hizi tungu
  ni kweli mtani umeasimika
  na ni wengu tulikuwa tunakukumbuka.

  ReplyDelete
 2. Mtakatifu Simon mmmmmmmmh!

  Da Yasinta mambo yamekuwa mengi. Hata hivyo nitajitahidi kuandika kila nipatapo wasaa.

  ReplyDelete
 3. kaka nakuandikia,
  diwani imetungika,
  fani yake muafaka,
  ujumbe waeleweka,
  nia nami naiweka,
  jibulo kuliandika.

  ReplyDelete