Wednesday, February 2, 2011

I wapi?

Ile ahadi yako,
Kuwa tungekuwa pamoja,
Kwa shida ama raha,
Ungenishika mkono,
Kwa mwambo,
Kwa machweo,
Kwa mawio,
Unishike mkono,
Nichechemee.

Ile ahadi yako,
Kuwa tungekuwa pamoja,
Tambarare ama kilimani,
Ungenishika mkono,
Jangwani,
Nyikani,
Ama baharini,
Unishike mkono,
Nisizame.

I wapi?
Nioneshe sasa!

3 comments:

 1. Fadhy mtani polepole ni mwendo yupo sehemu huyo unayemlilia na siku moja atakuja na mtashikana mikono utafurahi,atafurahi na mtafurahi. Ujumbe huu naona utamfikia tu.

  ReplyDelete
 2. Wapi ulipo kigoli, mpaka unanitupa,
  kumbuka yako kauli, awali uliyonipa,
  sasa u lile jabali, niwezalo kulitupa,
  yoyote iwayo hali, msaada uliapa,
  msaliti wa awali, bora dagaa si papa.

  ReplyDelete
 3. kazi safi ndugu yangu. usiwe na wasiwasi bratha.

  ReplyDelete