Thursday, September 23, 2010

Nafikiri

Akili si huru tena,
I mzigoni ikitafakari,
Ya leo ama ya kesho,
Ya mustakabali.
Mbiu ishapigwa,
Kitambo sasa.
Si ya mavuvuzela,
Bali ya awamu na dawamu.

Mwalimu darasani,
Alishasema,
Kupanga ni kuchagua.

Mahotma akatuambia,
Tuwe yale,
Mabadiliko,
Ambayo tungependa,
Kuyaona,
Duniani.

Sheikh Ebrahim Hussein,
Akainunua saa yake,
Alipoitazama vema,
Hakusita kusema,
Wakati ni Ukuta.

Namfikiria tena,
Mwanamapinduzi yule,
Bob Marley,
Kwa nini alisema,
Wakati Utaongea.
Kwa nini lakini,
Kazi ipo!

Msakatonge,
Mohamed Seif Khatib,
Akasema,
Hatukubali.
Kuja tena ili kuonewa,
Ndani ya nchi yetu,
Iliyo huru.

Akaja naye Ustaadh,
Khamis Amani,
Nyamaume,
Yeye akasema,
Mjinga mpe kilemba,
Mbele akutangulie.

Jinamizi bado laja,
La Ali Salim Zakwany,
Manenoye kugongana,
Bue silione bue,
La taji na buibui.

Nafikiri!

2 comments:

  1. Nadhani nitaungana nawe na kufikiri lakini labda tusifikiri sana sijui kama muda wa kufikiri unatosha. Bonge la fikra kwa alhamis ya leo.

    ReplyDelete