Sunday, August 15, 2010

Nishike mkono

Upweke unaponiandama,
Nami kukosa pa kuegama,
Bado nahitaji usalama,
Hata tufani linapovuma,
Ninaponywa nalo neno jema,
Maana sitochoka mapema,
Ni sauti yenye kuchombeza,
Niipendayo kuisikiliza,
Dunia inaponiumiza,
Peke yangu mimi sitoweza,
Nishike mkono.

2 comments:

 1. mmhh! shairi la leo ni kiboko
  Mungu amekusikiliza maombi yako
  wala usiumie
  na wala haupo peke yako
  huoni ulivyozungukwa na ndugu pia marafiki?
  Haya pokea mkono wangu

  ReplyDelete
 2. Upweke umeutaka mwenyewe...kwanini uende Dodoma bila kuaga?

  ReplyDelete