Tuesday, May 11, 2010

Chatu na siafu

Porini
Ndiyo kule msituni
Kwenye miti
Na udongo wenye rutuba.
Haiyumkini,
Mwenye mabavu,
Akataka,
Kuonesha yaliyo wazi,
Na kuficha
Yaliyofichwa,
Pengine.

Mabavu,
Wala si hoja,
Mradi maarifa.

Wewe useme,
Sema tu.
Mdomo unao,
Wastara.
Jitutumue,
Haswaa,
Maguvu unayo,
Waama.

Wao waseme,
Watasema tu,
Sauti wanayo,
Waadhi.
Hawana maguvu.
Umoja wao
Ndiyo silaha yao,
Watashinda.

Maana ilisemwa,
Kale na sasa
Wema,
Hushinda uovu.

4 comments:

 1. MTANI HIYO PICHA YAKO HAPA KOFIA NA SKALF BOMBI KWELI. IMENIVUTIA KWELI...!!
  UMIPENDEZA NTANI!!

  ReplyDelete
 2. Shairi zuri. Japo chatu limekakawana, naamini siafu hawajakata/hawatakata tamaa....

  ReplyDelete
 3. ´´Maana ilisemwa,
  Kale na sasa
  Wema,
  Hushinda uovu. ``- Umemaliza Mkuu

  ReplyDelete