Tuesday, April 27, 2010

Wewe tu

Mpenzi wangu sikia,
Maneno ninayokwambia,
Kwamba nakupenda,
Wewe.
Nitakuja hadi kwenu,
Niwaone wazazi wako,
Niwaambie nakupenda,
Wewe.

Niahidi utanipenda,
Siku zote maishani,
Kwa kuwa nakupenda,
Wewe.
Kwangu hakuna mwingine,
Nitayempenda zaidi,
Niamini nakupenda,
Wewe.

Najisikia fahari,
Ninapopendana nawe,
Nitazidi kukupenda,
Wewe.
Sogea karibu nami,
Nilipate pendo lako,
Nizidishe kukupenda,
Wewe.


Nililiandika shairi hili nikiwa kidato cha tano pale Mkwawa High School. Nimeona si vibaya nikiliweka jamvini hapa.

2 comments:

 1. Hujafanya vibaya kabisa kuweka hapa hili shairi.
  Fadhy naamini mpenzio amekusikia
  Siku moja atasogea na mtakuwa pamoja
  Mola aanakusia ombi lako kwani unaomba mno.
  Nakutakia kila la kheri mpenzio akusie na muwe pamoja.

  ReplyDelete
 2. hata kama ungeandika miaka 2000 ilopita bado maudhui yake yako palepale.

  safi thana!

  ReplyDelete