Monday, April 19, 2010

Wakati

Wahenga ati walisema
Wakati,
Ni ukuta.
Wahenga hawa
Walijawa busara.

Ati wakaongeza,
Kuwa
Mpiga ngumi ukuta,
Huumiza
Mkonowe.

Aisee!

Nani awezaye
Rusha yake ngumi?
Ukutani,
Akabaki salama.
Atoke wapi?

1 comment:

  1. hapa pazuri sana kila ukipita unafaidi. Ahsante sana.

    ReplyDelete