Thursday, March 11, 2010

Njoo nikwambie

Moyo wangu umenituma....
Hili neno nije kusema......
Moyo wahitaji kutuwama.....
Kwa moyowo ulo mwema.......
Moyo sasa unatamani......
Pendo lako la thamani.......
La pekee humu duniani......
Zawadi kutoka kwa Maanani......
Moyo wala hauna shaka.....
Kwani kwako umefika.....
Moyo wataka burudika.....
Kwa penzi lisomithilika.

6 comments:

 1. Nami naitika.....
  Sema hilo neno....
  Ili moyo wako utuwame....
  Wala usipie mayowe....
  nami moyo watamani...
  Nawe pendo lako la thamani...
  Pia la pekee kote ulimwenguni...
  Na pia ni zawadi....
  Ni vizuri kama moyo hauna shaka....
  Nami nakukaribisha...
  Burudika utakavyo....
  Kwa vyovyote utakavyo

  ReplyDelete
 2. Hakika nimekusikia....
  Hivyo napa nakungojea.....
  Siachi mie kukuwazia.....
  Hadi utakapotokea.

  ReplyDelete
 3. Mbona nami natamani...
  Mwanitia majaribuni...
  Ninaogopa jamani...
  Kudondokea penzini...
  Nikimweka moyoni...
  Nitakuwa kifungoni...
  Nikimtoa mawazoni...
  Maumivu mtimani....

  ReplyDelete
 4. These are the two best poems EVER written:

  http://pichazakikubwa.blogspot.com/2010/03/best-poem-ever-written-i.html

  http://pichazakikubwa.blogspot.com/2010/03/best-poem-ever-written-ii.html

  ReplyDelete
 5. Sijui mie nsemeje sasa :-)

  usowadhania kuwa si washairi kumbe ndo duh!

  Papa Fadhy, usipoangalia unaweza kujikuta ukitupwa nje ya ulingo!

  ReplyDelete
 6. kadinali Ng'wanambiti nami nimeona kuna watu wanakuja kasi na si ajabu wakanivua crown. wacha nami niingie kambini kujifua ili wasinipore.

  ReplyDelete