Saturday, January 2, 2010

Mwaka Mpya

Mwaka mpya umefika,
Mungu tunamshukuru,
Maana yeye ndiye kapenda,
Mwaka huu kuuona,
Tunasema ahsante.

Wengi walipenda,
Lakini hawakuweza,
Kuiona nuru mpya,
Yake mwaka mchanga,
Hawakuweza kabisa.

Si kwamba tu wema,
Hatuna mema hata kidogo,
Ila ni mapenzi yake,
Muumba wa mbingu na dunia,
Hakika ni mapenzi yake.

Tuzidi mwomba yeye,
Atujaalie zaidi na zaidi,
Ili tuweze kuiona,
Miaka mipya mingi mingine,
Maana yeye ndiye awezaye.

Heri kwenu nyote!

2 comments:

 1. Nanukuu "Si kwamba tu wema,
  Hatuna mema hata kidogo,
  Ila ni mapenzi yake,
  Muumba wa mbingu na dunia,
  Hakika ni mapenzi yake" mwisho wa kunukuu. Nami nasema Amina.

  ReplyDelete
 2. heri ya mwaka mpya na kwako pia uwe mwaka wa mafanikio pia afya njema kwao na familia kwa ujumla

  ReplyDelete