Sunday, September 20, 2009

Utu wema

Ndiyo haswa sifa yako,
Iliyo moyoni mwako,
Wema kwa rafiki zako,
Mola amekujalia.

Wema wako wa moyoni,
Ni kitu chenye thamani,
Mwinginewe hafanani,
Hakika najivunia.

Wema wako wenye dhati,
Usiojali wakati,
Wema mwingi kibati,
Yeyote kufurahia.

Roho yenye utajiri,
Nzuri kushinda johari,
Kuwa nawe ni fahari,
Kwa maisha ya dunia.

Umepewa utu wema,
Wenye thamani daima,
Moyo wangu wanituma,
Sifazo kukupatia.

Kwa Mola nakuombea,
Azidi kukupatia,
Heri na fanaka pia,
Katika hii dunia.

6 comments:

 1. Shairi nzuri hili Uwe mwema nawe pia mtani. maneno mazuri sana umeyaandika.

  Nimenukuu "Wema wako wa moyoni,
  Ni kitu chenye thamani,
  Mwinginewe hafanani,
  Hakika najivunia."

  ReplyDelete
 2. Utu wema ni muhimu,walowengi takupenda,
  Pindi yajapo magumu,tasaidiwa kushinda,
  Talindwa ulio tunu,hakuna taye kuwinda.


  Heko kaka Fadhy.

  ReplyDelete
 3. Great blog!!
  If you like, come back and visit mine: http://albumdeestampillas.blogspot.com

  Thanks,
  Pablo from Argentina

  ReplyDelete
 4. Bomba la shairi hili Papaa Fadhy!

  Chakusikitisha ni kwamba watu huwa wanangoja kumwambia mtu haya akiwa hai mpaka wasubiri kudai Marehemu alikuwa mtu mzuri!

  ReplyDelete