Wednesday, September 30, 2009

Mwisho wa mwezi

Mwisho wa mwezi ni mambo, tena kubwa burudani,
Mfukoni hakujambo, na raha hadi moyoni,
Pesa sabuni ya roho.

Pesa sabuni ya roho, nazo siku zimefika,
Pesa inao uroho, tamaaye kuzishika,
Tamu za mwisho wa mwezi.

Tamu za mwisho wa mwezi, kwani ushazisotea,
Umefanya sana kazi, hakiyo wakikugea,
Ifurahi familia.

Ifurahi familia, rudi nyumbani mapema,
Pesa ikikuzingua, kwenye shimo utazama,
Eti pesa ni shetani.

Eti pesa ni shetani, hasa ukishazipata,
Hulali hata nyumbani, matako kulia mbwata,
Mfalme ndiyo wewe.

Mfalme ndiyo wewe, na kizungu waongea,
Na hadhira usikiwe, na sifa kukutolea,
Huo ndo mwisho wa mwezi.

Huo ndo mwisho wa mwezi, wa mwingi umaridadi,
U chakari hujiwezi, kichwa maji kuzidi,
Akibayo kukauka.

Akibayo kukauka, hujali kuhusu kesho,
Wewe ni wa uhakika,
Mwezi ufikapo mwisho,
Mwisho wa mwezi ni raha.

3 comments:

 1. Ni kweli kaka si hwudesi nda.hongerazokwa kutukumbusha

  ReplyDelete
 2. uhongise kwa hili, mie ndo kwanza mfuko umeshatoboka....LOL

  ReplyDelete
 3. Mwisho wa mwezi bwana,kila mmoja atataka kuwa karibu yangu, utawasikia, mbona siku hizi huonekani, wengine watataka kuja kurekebisha ukosi wa shati,hata kama umekaa vizuri,yani lengo likiwa ni kuwa karibu yangu, kisa mwisho wa mwezi!
  Mambo ya mwisho wa mwezi haya.

  ReplyDelete