Tuesday, September 1, 2009

Mlevi na Falsafa yake

Kwamba asiyejua,
Na hajui kwamba hajui
Ndiye mwerevu zaidi,
Hapa duniani,
Wataka kushangaa?

Bora asiyejua,
Na anajua kwamba hajui,
Kwani tungesemaje?
Ilhali wengine,
Wametuvisha vidoto!

Wasomi na wanasayansi,
Nd'o walogeuka,
Wamekuwa wanasiasa
Sasa wameshatonoka
Wakukumbuke wewe,
Kwa lipi hasa
Ulilonalo?

Maana ya maneno:
Vidoto - vipande vya nguo maalumu wafungwavyo ngamia machoni wasafiripo jangwani.
Tonoka - kuwa na hali nzuri kwa sababu ya mafanikio fulani.

6 comments:

 1. Kazi nzuri Fadhy, je huwezi kuanzisha darasa na wengine tuje kujifunza jinsi ya kuandika haya mashairi maana usomapo utamu mpaka kidole gumba la mguu:-)

  ReplyDelete
 2. Namuunga Simon hapa... DUH! Serina

  ReplyDelete
 3. Da Yasinta itabidi nifungue darasa ili ufaidike.
  Mtakatifu Simioni......tupo pamoja mkuu............duh....!!!!!!
  Da Serina umeadimika muno, nini kinakusibu? Nimeyamiss mashairi yako matamu.

  ReplyDelete
 4. Vidoto na tonoka, mh. Lakini ninachoshukuru nilifaulu mtihani wa kiswahili wa kidato cha nne!!

  ReplyDelete
 5. Hongera sana kaka Chib kwa kufaulu mtihani wa Kiswahili kidato cha nne. Pia shukrani mara alfu lela ulela kwa kutochoka kunitembelea.

  ReplyDelete