Tuesday, August 11, 2009

Heri umoja

Naliandika shairi, kwa vyama vya upinzani,
Viongozi wafikiri, wafikiri kwa makini,
Maana mambo si shwari, mageuzi hatuoni,
Wakati umeshafika, twataka mabadiliko.

Wenyewe mkilumbana, mshindwe kuwa wamoja,
Watawala hukazana, kuziuwa zenu hoja,
Mnapaswa kupambana, tumeshachoka kungoja,
Twataka mbadilike, yawe mageuzi kweli.

Zilizopita chaguzi, kushinda hamkuweza,
Twalaumu viongozi, kote walikoteleza,
Tatizo lingali wazi, umoja mwatelekeza,
Ni ngumu ninyi kushinda, msipotaka umoja.

Umoja huleta nguvu, hivyo nanyi unganeni,
Msioneane wivu, haya mambo jifunzeni,
Maana ni upumbavu, mnazidi shuka chini,
Umoja wawezekana, mkiwa na nia moja.

Kwa kila mtu na lwake, mtazidi kuchemsha,
Vema jambo lifanyike, vinginevyo mtakesha,
Na mwakani muanguke, kwa anguko la kutisha,
Hima amkeni sasa, wakati hausubiri.

Wala kura siyo chache, ila mwagawana mno,
Ubinafsi muache, na mshikane mikono,
Na hilo tusiwafiche, ushindi huwa mnono,
Si ndoto za alinacha, amkeni usingizini.

Wananchi wawapenda, ila hawana imani,
Vyamani mnavurunda, niaje madarakani?
Kama mwataka kushinda, basi hebu unganeni,
Nasi tutawapa kura, mtashinda kwa kishindo.

Nyote mwataka gombea, dunia hay'endi hivyo,
Umoja mkiwekea, kama sisi tutakavyo,
Kura tutawapatia, vyovyote vile iwavyo,
Hima ninatowa wito, wapinzani unganeni.

Mjuwe chama tawala, hakilali usingizi,
Vipi ninyi mnalala, mmeshamaliza kazi?
Mtazishindaje hila, umoja hamuuwezi?
Mtazidi kuchemsha, kama msipoungana.

Kaditama nimefika, ni beti kumi kwa leo,
Ujumbe niloandika, ubadili mwelekeo,
Ili hatamu kushika, yahitajika upeo,
Umoja ndiyo silaha, kwani umoja ni nguvu.

6 comments:

 1. Mwananchi wewe. Waendelee kuelimika japo hawatakiri. Ni wajinga wa fukara zao na hawataweza kuamini kuwa kuna suluhisho katika masuluhisho waonayo. Hivyo hawatasaka suluhisho zaidi ya kusaka umaarufu. Bob alisema "see they want to be the stars, so they fight the tribal war"
  Let's keep on lighting their minds.
  TIME WILL TELL

  ReplyDelete
 2. Ahsante sana kaka Chib, da Yasinta, Mtakatifu Simon (aliyenivika daraja la uaskofu) na kaka Mubelwa.

  Wakati fulani siasa za vyama vya upinzani na Tanzania kwa ujumla huchefua.

  Sijui wana tatizo gani?

  Ubinafsi.

  Wakiuacha huo, tutapiga hatua.

  ReplyDelete
 3. Reckon a note Our Nightfall darkness Prices at www.Pharmashack.com, The Aberrant [b][url=http://www.pharmashack.com]Online Dispensary [/url][/b] To [url=http://www.pharmashack.com]Buy Viagra[/url] Online ! You Can also Earwitness Humongous Deals When You [url=http://www.pharmashack.com/en/item/cialis.html]Buy Cialis[/url] and When You You [url=http://www.pharmashack.com/en/item/levitra.html]Buy Levitra[/url] Online. We Also Be subjected to a Basic Generic [url=http://www.pharmashack.com/en/item/phentermine.html]Phentermine[/url] As a constant expenses to Your Nutriment ! We Up Mark chic [url=http://www.pharmashack.com/en/item/viagra.html]Viagra[/url] and Also [url=http://www.pharmashack.com/en/item/generic_viagra.html]Generic Viagra[/url] !

  ReplyDelete