Tuesday, August 18, 2009

Haya sasa

Mpira uliochezwa, umefika ukingoni,
Mpira umemalizwa, dakika zake tisini,
Kwa wale waliolizwa, warudi tu majumbani,
Maana imeshaelezwa, upinge wewe ni nani?
Kazi sasa imekwisha, twendelee na mengine.

Na refa ndiye mwamuzi, akisema imetoka,
Kama kamaliza kazi, kwamba ana uhakika,
Hajui yako majonzi, hajui wahuzunika,
La kufanya huliwezi, ni lazima kuridhika?
Kwani dua lake kuku, halitompata mwewe!

5 comments:

 1. Unafikiri waliopoteza mechi wamefurahi? Ni swali tu ambalo halihitaji jibu, maana jibu kila mtu analo jibu la kwake!

  ReplyDelete
 2. Mmmmh haya mambo ya mpira mi sisemi kitu leo.la tupo pamoja!!!

  ReplyDelete
 3. Mchezo uliochezwa , umefika ukingoni.
  Ingawa umemalizwa, tuko bado ulingoni
  Ndio leo tumelizwa,kesho tuko ulingoni
  Kesho utastukizwa,kombe twalo kibindoni

  Kazi haijakwisha, si lazima kuridhika


  DUH!

  ReplyDelete
 4. Wala mimi sikujua, Kitururu mshairi,
  Ni leo nimegundua, naona sana fahari,
  Hongera sana.

  Kuhusu huo mpira, ni lazima tutashinda,
  Wala hatuna papara, ingawa hatujapenda,
  Ni hayo tu!

  ReplyDelete
 5. Inawezekana ni mengi hujui kuhusu Mtakatifu Simon mtani:-)

  ReplyDelete