Thursday, July 2, 2009

Kipaji kipya

Vita

Vita inapotokea, wananchi hukimbia,
Wananchi huumia, bila hata ya hatia,
Watoto wanaumia, hata wanawake pia,
Watu wote Afrika, tupinge vita jamani.

Sarah Victor Ngwale.

Leo majira ya jioni nilikwenda Tabata Segerea kuitembelea familia ya mjomba wangu. Nimepigwa na mshangao kumkuta binamu yangu Sarah mwenye umri wa miaka 12 akiandika mashairi. Binamu yangu huyo anasoma darasa la VII shule ya msingi Tabata Segerea. Nikamwomba aniandikie beti moja kuhusu jambo lolote. Wakati huo huo TBC1 wakawa wanaonesha wakimbizi wa Kongo. Akaniambia anaandika kuhusu vita. Nimefurahi sana kupita ninavyoweza kueleza kugundua kuwa nina mrithi. Namwombea kila la kheri katika masomo yake, na katika mitihani yao ijayo ya taifa. Afanikiwe daima.

6 comments:

 1. Binamu kazi aweza, kaka fadhy nakwambia.
  kipaji kuendeleza,binafsi nashadadia.
  vita shairi kawaza,sichoki kumsifia.
  yaliyopo atujuza,hongera nampatia.

  ReplyDelete
 2. Nilijua ni wewe umeandika. Kwa kweli huyu binti ana kipaji kama binamuye. Msalimie na mwambi kazi nzuri sana.

  ReplyDelete
 3. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 4. Hongera Dada Sarah Victor Ngwale!

  Papaa Fadhy sasa usihofu kuhusu Mrithi!:-)

  ReplyDelete
 5. Tunamtakia kila la heri, lakini lazima akuzidi wewe ndio itakuwa furaha yetu :-)

  ReplyDelete
 6. Ahsante sana mkuu Kissima, da Yasinta, Papaa Simon na mkuu Chib kwa kukikubali kipaji hiki. Huwa nalisoma hili beti kila siku na kubaki na kinywa wazi. Nami furaha yangu ni kuwa aandike zaidi na zaidi. Hadi hapo nadhani keshaonesha dalili ya kunifunika muda si mrefu. Nami ntajitahidi afanye hivyo.
  Nawashukuruni sana wadau kwa maoni yenu.
  Pamoja sana!

  ReplyDelete