Friday, July 10, 2009

Ilani

Kitanda usikiache, nje ukakimbilia,
Ukatema zako cheche, kwingine kuzitumia,
Usipandikize miche, holela kujiotea.

Pia usingoje kuche, ili uruke na njia,
Nyumbani usikukache, mbali kukakunogea,
Nje usiwapekeche, wako nani wamwachia?

Hiyo ya nje mikweche, shida itakuletea,
Itasababisha wiche, ukabaki jijutia,
Usijifanye mkoche, huko ukachokonoa.

Maisha ni siku chache, ndani ya hii dunia,
Chakula cha nje kiache, wadudu wameingia,
Ni kheri nisikufiche, kwa maneno kukwambia.

7 comments:

 1. Det är sant man lever bara en gång här i jorden. Tack för den fina dikten.

  ReplyDelete
 2. Ni kweli da Yasinta, binadamu huishi mara moja tu katika hii dunia.
  Nami nakushukuru sana kwa nasaha zako muktadha.

  ReplyDelete
 3. Hapana kurukaruka, takuja kuanguka.
  Wadudu tawakaribisha,maisha kuyafupisha.
  Ile moja anatosha,
  nje takanyaga miwaya.

  ReplyDelete
 4. Hapana kurukaruka, mwishowe uta anguka.
  Wadudu tawakaribisha,maisha kuyafupisha.
  Ile moja anatosha,
  nje takanyaga miwaya.

  ReplyDelete
 5. Mtanga kamaradia
  Ukweli umewasilia
  Faida kutugawia
  Ujumbe kutumwagia

  Naomba nikusaili
  Kidogo sekunde mbili
  Vibaya kushika mbili
  Kama ndumilakuwili

  Ukweli wajulikana
  Kitanda kukikana
  Mbona bado twabanana?
  Wengine kushikamana!

  Kuchovya kubaya sana
  Hili twalijua sana
  Bado najiuliza sana
  Mbona twachovya sana?

  ReplyDelete
 6. Yasinta tumesikia,
  Ni kweli kwenye dunia,
  Mara moja hutokea,
  Kamwe haitorudia.

  Kissima mwenye hekima,
  Uzuri nimekusoma,
  Ni vema watu wazima,
  Haya tukayasikia.

  Usigune Mumyhery,
  Vema watu wafikiri,
  Nyendo nyingi siyo nzuri,
  Kisha kesho kuumia.

  E Mwanasosholojia,
  Ujumbe naupokea,
  Na wote wamesikia,
  Ni vema kutorudia.

  ReplyDelete