Thursday, June 18, 2009

Wasiwasi wa nini?

Wasiwasi wako ni wa nini?
Au ni kwamba hujiamini?
Wewe kuwa na raha moyoni,
Kwani mwingine simtamani....

Nakupenda hunacho kifani,
Nadhiri naiweka moyoni,
Hadi siku nafukiwa chini,
Nitakupa pendo la thamani....

Mwingine wala simbaini,
Watosha vema mwangu rohoni,
Huwa nahisi nipo peponi,
Kila uwapo mwangu pembeni....

Ondoa wasi huo moyoni,
Kuwa na furaha maishani,
Nifae rahani na shidani,
Nijaze ndani mwako moyoni.

3 comments:

 1. Mmmhhh.Hongera kwa huyo umpendaye
  kwani inaonyesha unampenda kweli
  hadi wivu namwonea
  kweli watu wanajua kupanda
  ni hayo tu.

  ReplyDelete
 2. Wasiwasi wataka jua ni wa nini,
  Ni kuwa mwenyewe hajaamini,
  Umempenda kajiona labda ni chizi,
  Pendo na furaha hajazoea maishani.

  ReplyDelete
 3. Yasinta mapenzi kwake hayana kipimo,
  Ni zaidi ya maneno ya wangu mdomo,
  Kwake nimeweka msimamo.

  Serina kwanini hataki amini?
  Nimemwambia tokea zamani,
  Yupo pekee mwangu himayani.

  ReplyDelete