Wednesday, June 17, 2009

Ulimi!

Huwaponza watu sana...
Huleta kuchukiana...
Watu wakishagombana...
Huleta kubaguana...
Na watu kusengenyana...
Kiungo kidogo sana...
Familia kulumbana...
Na ndugu kuchukiana...
Na kudharauliana...
Mataifa kupigana...
Hata watu kuuana...
Na wapenzi kuachana...
Marafiki kukosana...
Kushindwa salimiana...
Ulimi.

4 comments:

 1. Ulimi huo.
  Natumaini siku nyingine utatutolea na upande wa uzuri wa ulimi!!

  ReplyDelete
 2. Ni kweli ulimi hauna mfupa. Na kibaya zaidi ukisemacho huwezi kurudisha tena.

  ReplyDelete
 3. Ulimi ni kinyama kidogo sana lakini hatari yake ni kubwa ukitumika visivyo, bali ni kinyama chema kikitumika vilivyo.

  Watu huweza kuangamia kwa kutumiwa vibaya, bali watu wanaweza kuongolewa kwa kutumia kinyama hicho kwa wema.

  Muhimu ni kuchunga ndimi, zi2miwe kwa maslahi na matlaba adhiim kwa mustakabali mwema katika jamii.

  Wakatabahu

  ReplyDelete
 4. Kaka Chib,
  Upande wa uzuri wa ulimi....ntausema siku moja. Maana upande huo humtoa hata nyoka pangoni.

  Da Yasinta, shukrani mara milioni kwa kunitembelea mara kwa mara.

  Kaka Mkwinda, u khali gani? Mbeya kuaje? Shukrani sana kwa maoni yako.

  ReplyDelete