Friday, June 26, 2009

Pumzika kwa amani

Mshumaa umezima,
Moyowo ulipogoma,
Mautini ukazama,
Basi uende salama.

Hatutokuona tena,
Tuliokupenda sana,
Tunamwomba Maulana,
Akuweke pale pema.

Tutakumbuka thriller,
Hakukuwa na kulala,
Yapendwa kote mahala,
Basi uende salama.

Nenda Mike salama,
Ni ghafla umezima,
Kwa'o moyo wako mwema,
Ulale mahala pema.

Amina.

2 comments:

 1. Apumzike kwa amani,
  mengi ya maishani,
  ametuchia duniani,
  Mike buriani,
  tutammisi jukwaani,
  tutamsikia redioni,
  tutamwona kwenye televisheni,
  mashairi yake nawa'mbieni,
  yatabaki akilini,
  kapoteza uhai,
  kazi zake hakika bado zi hai.

  ReplyDelete