Friday, March 27, 2009

Wewe

Wewe kwako nilofika, shairi nakuletea,
Moyo wangu tele shaka, wenda mbio peapea,
Mapenzio nayasaka, toka zama watambua,
Mbona unaninyanyasa, kwa ahadi ziso timu,

Huishi kunishutumu, ya kwamba sijatulia,
Nifanyeje mahamumu, upate kunielewa,
Utaja kujilaumu, vile unanitendea,
Nasubiri pasi jaka, iko siku utajua,

Maisha chombo bahari, siku kasi makasia,
Sina jambo kusubiri, shaka ipo kwa dunia,
Itaja isidhahiri, roho hatima ingia,
Taenda nayo sononi, upweke wa huba yako,

Yako hapa mawazoni, mapenzi yasiyo shaka,
Sitoacha abadani, ahadi nimeiweka,
Uje leo ukongweni, aipendapo rabuka,
Yakishindwa duniani, nitakugea ahera.

Kwa moyo wote!

3 comments:

 1. Beti za shairi kwa kweli zinasema mengi na zinaingia mpaka rohoni kabisa. yaani zimenigusa sana.kazi nzuri mtani!!

  ReplyDelete
 2. ahsante sana mtani kwa kunitembelea mara kwa mara. mambo vipi huko uliko?
  kuna ulanzi huko?

  ReplyDelete
 3. Ulanzi haumalizi karibu sana.Unataka nusu robo au:-)

  ReplyDelete