Monday, March 23, 2009

mwananchi mimi

Umepita muda niloahidi,
Hakuna dalili ya kurudi,
Walau salamu,
Ningefanyaje?

Mwanikumbuka?
Au siasa zimewapa ahadi mpya,
Mkasahau yote,
Poa.

Sipo mbali nanyi wenzangu,
Nimetamani nami nirudi,
Niwe hai au mfu,
Mtaona!

Fikra zenu ndilo tukio,
Ninalo litaraji,
Ninazo hazijanitoroka,
Zangu mie.

Fikra zangu zifike kwenu,
Ziwagutushe,
Walolala ziwaambie,
Vukani!

‘Kwa wenye mioyo safi’

1 comment:

  1. Fadhy karibu sana tena kijiweni binafsi nimekumiss na pia nimemiss sana kusoma mashairi yako mazuri huwa yananipa faraja. ni hayo tu

    ReplyDelete