Thursday, December 18, 2008

Nataka kusema kitu

Nataka kusema kitu, bado nakifikiria,
Nifikiri mara tatu, kisha nitawaambia,
Ninachotaka kusema.

Nimepatwa na ufyatu, mambo yamenizidia,
Msiotwe roho kutu, mwapaswa nisaidia,
Kuna kitu ntasema.

Miaka makumi tatu, mie naikaribia,
Nami kati yao watu, heshima naitakia,
Mwaelewa nachosema?

Na huu siyo upatu, nikaukurupukia,
Nitawashangaza watu, ovyo kujiamulia,
Niendelee kusema?

Moyo wangu siyo butu, pekee kujikalia,
Nao wahitaji kitu, kesho nitawaambia,
Basi kesho ntasema.

3 comments:

 1. Sema ni nini, kinakusumbua,
  Tutasikiliza, na tutakusaidia,
  Usiposema, hatuwezi kujua,
  Ni nini unawaza.

  ReplyDelete
 2. Sitoi maoni mpaka kesho ifike. Ntatoa kwa kinachoelezwa. Sasa wacha nitegeshe, ili kabla ya kuamka niwashe kompyuta na kabla sijafungua macho nianze kusoma.
  Hahahahahaha
  Tuko pamoja Kaka

  ReplyDelete
 3. Fadhy HONGERA sana kwa hiyo miaka makumi tatu. Ngoja nikuimbia kidogo happy birthday to ux2 Happy birthday u Fadhy happy birthday 2 u. Happy birthday Fadhy.

  ReplyDelete