Saturday, December 27, 2008

Karibu sana Yasinta

Karibu sana nyumbani, karibia Tanzania,
Sote tupo furahani, kwa hamu twakungojea,
Hakika twaitamani, siku hiyo kuwadia,
Karibu sana Yasinta.

Warudi kutoka mbali, mbali sana na nyumbani,
Twafurahi kila hali, nyumbani kupathamini,
Ukiwa mbali mahali, hujiona ugenini,
Karibu sana Yasinta.

Nyumbani jama pazuri, nyumbani panayo raha,
Mwenyewe hebu fikiri, nyumbani huwa furaha,
Ukifika utakiri, nyumbani siyo karaha,
Karibu sana Yasinta.

Yasinta tunakungoja, uzilete changamoto,
Yasinta mwingi wa hoja, tena hoja moto moto,
Kwetu u kama daraja, ili tuuvuke mto,
Karibu sana Yasinta.

Nyumbani usipachoke, maana panapendeza,
Hata kesho pakumbuke, usije kupatelekeza,
Tena pana raha yake, na tena tutakutuza,
Karibu sana Yasinta.

Karibu sana Yasinta, twakukaribisha sote,
Nyumbani utatukuta, nasi furaha tupate,
Na jasho tutakufuta, tunapaswa tukufute,
Karibu sana Yasinta.

KARIBU SANA NYUMBANI.

3 comments:

 1. asante sana kwa ukaribisho wako,
  yaani hizo beti zako
  umezitunga kwa makini na moyo
  nami nasema asante sana fdhy

  hapa nilipo ni furaha sana
  kuja nyumbambani tanzania
  kuonana na ndugu, marafiki na jamaa
  nami nasema asante sana Fadhy


  Je nimeweza au

  ReplyDelete
 2. nimelipenda sana shairi hili, kwa kweli watu wana vipaji. Mungu akulinde fadhy Mtanga. Asante sana tena sana. ubarikiwe sana. Tutaonana

  ReplyDelete