Monday, December 15, 2008

Alaa Kumbe!

Asubuhi waamka,
Waanza kukuna kichwa,
Unawaza,
Utawaza sana!
Ukipata jawabu,
Heko nyingi.

Jana,
Hukuyamaliza yalojiri,
Ungeyamaliza vipi?
Uwezo hukuwa nao,
Kwa nini?
Najua huna jibu.

Maisha!
Kwani ni nini?
Ama yana nini?
Utawaza sana,
Nami nawaza sana,
Ala kumbe?
Kumbe nini?

Wajiuliza mara mia,
Uwape tena?
Lipi jipya litakuja?
Ngoja kidogo.
Maisha, maisha,
Yanakwisha,
Usiseme hivyo,
Nisemeni?
Sijui.
Hayo madaraka,
Tumewapa,
Wengine wakachukua bila kupewa,
Nini chanzo?
Pengine tamaa.
Tulikuwa na matarajio,
Eti eh!

Matarajio?
Ya nini tena,
Kwenu hamli?
Hapana.
Sasa nini?
Hali bora.

Alaa kumbe!
Ikawaje sasa?
Hatuhitaji kukujibu,
Maana hali yenyewe,
Mwenyewe si unaiona?

Hapana sioni kitu,
Ni kweli,
Huoni kitu ingawa una macho,
Machoyo mapambo,
Huwezi ona lolote,
Kwa kuwa,
Hupendi kufanya jitihada,
Jitihada? Za nini tena?
Katika kufikiri.

Mmh!
Sote tukaguna.

7 comments:

 1. Katika maisha watu tumeachana sana, sio wato waoamka asubuhi na kuanza kukuna kichwa, Wote tunawaza tofauti wengine hawawezi kuwaza kabisa vipi watayajenga maisha yao na kinyume wengine wanawaza mpaka maumivu ya kichwa yanawapata. Hivi ndivyo nilivyoelewa sijui kama naeleweka!!kazi kwelikweli

  ReplyDelete
 2. Fadhy kazi nzuri sana kijiji kinapendeza maana Mmh safi sana natamani nihamie huko

  ReplyDelete
 3. ahsante sana kwa pongezi zako. nimejaribu leo kujifunza kupamba ingawa siyo fani yangu. vipi kimependeza?

  ReplyDelete
 4. Kazi nzuri malenga. Nikuulize swali: KUna mahali umeanza kukitumia vyema kipaji hiki zaidi ya hapa kwenye blogu?

  Kqazi zako zimesimama wima! Heshima sana mkubwa. Napenda sana mashairi na lyrics ingawa sina uwezo mzuri wa kuyaandika. Ila nikiyakutaga yameandikwa, du! Msisimko.

  ReplyDelete
 5. Maisha?
  ngojea nikunukuu;'''Mmh!
  Sote tukaguna.''

  Umenifikirisha sana Mkuu!Asante!

  ReplyDelete
 6. Da Yasinta, nakushukuru sana kwa kuikubali kazi hii ambayo ni karama kutoka kwa Mungu.
  Kaka Bwaya, hiki kipaji...mh, nakitumia tumia ila zaidi kwenye hii blog. Nakushukuru sana kwani naamini unaikubali kazi hii.
  Kaka Kitururu, nafurahi kuwa lengo langu limetimia. Niliandika shairi hili ili atayelisoma afikirie sana.
  Nakushukuruni sana nyote muitembeleayo blog hii.
  Wacha tuseme, tutasema pasi kuchoka, kwa sababu inatulazimu kusema. Tusiposema, nani atatusemea?

  ReplyDelete