Wednesday, December 31, 2008

Ahsante sana Mungu

Siku muhimu 'mefika,
Mwaka unamalizika,
Ni mbali tulikotoka,
Mola katupa baraka,
Ni wengi hawajafika,
Ahsante sana Mungu!

Eeh Mola tupe karama,
Tujalie yale mema,
Uzidi tupa uzima,
Mwaka uishe salama,
Mola mwingi wa Rehema,
Tunakushukuru sana!

2 comments:

  1. Ni kweli na vema kumshukuru mungu kwa yote aliyotutendea. wengine huwa hawabahatiki kufika hata siku moja Asante sana mungu

    ReplyDelete
  2. salam from khudori. your can read my post by Google translate in my site

    ReplyDelete