Tuesday, June 5, 2007

ada ya mja

Hili linawezekana, ijapokuwa ni gumu,
Na halitoshindikana, ndiyo yetu majukumu,
Nitakufundisha sana, mi hapa ndiyo mwalimu.

Mimi sishindwi na kitu, sijawahi asilani,
Ncha yangu siyo butu, ina makali fulani,
Mimi ni mtu wa watu, tangia hapo zamani.

Kila kitu ninaweza, hakuna nisichojua,
Haya nayowaeleza, ndivyo itakavyokua,
Haswa nitatekeleza, tena kwa kila hatua.

Mja huongea hivyo, tena kwa kusisitiza,
Huaminika vilivyo, ni fundi wa kueleza,
Vyovyote vile iwavyo, husisitiza aweza.

Leo hivi kesho vile, alimradi maneno,
Tawapiga watu shule, kwa ahadi zake nono,
Mwishowe mbivu wasile, japo wamengoja mno.

2 comments:

  1. jamani! awali ilikuwa ni vigumu kuamini, sasa nimeamini kuwa ndiye fadhy tuliyesoma pamoja o' level. kumbe hujaacha kuandika mashairi. hongera sana best. hope utafika mbali sana.

    ReplyDelete
  2. hongerq sana dogo inaonyesha ni jinsi gani unavyotumia mda mwingi kufikiri mambo,keep it up,tuanze biashara best tuuze mashairi kwa wasanii wa bongoflava walio wavivu wa kutafuta mistari. Is me Niyukuli

    ReplyDelete